8 Novemba 2021 - 11:58
Kamanda Rashid: Maadui wasiujaribu uwezo wa IRGC na jeshi la Iran

Kamanda wa Makao Makuu ya Kamandi ya Kijeshi ya Khatamul Anbiya ya Iran amewatahadharisha maadui wa Jamhuri ya Kiislamu dhidi ya kuujaribu uwezo wa jeshi la nchi hii na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Meja Jenerali Gholam Ali Rashid alitoa indhari hiyo jana Jumapili wakati wa kuanza mazoezi ya kijeshi yaliyopewa jina la Dhulfiqar-1400 yanayofanyika huko kusini mashariki mwa nchi.

Amesema vikosi vya majeshi ya Iran daima vipo tayari kwa ajili ya operesheni zozote za kistarajia za kujibu chokochoko za maadui, na kuimarisha usalama, uthabiti na mamlaka ya kujitawala taifa hili, mkabala wa miungano ya maadui (hususan muungano wa Marekani na Wazayuni).

Kamanda Rashid ameeleza bayana kuwa,  vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vitatoa jibu mwafaka kwa uchokozi wowote wa madola ya kiistikbari na wavamizi kwa kiwango chochote.

342/